Kwaya ya Mt. Stefano Shahidi ilianzishwa mwaka 1975 katika Parokia ya Kipawa, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ikiwa na lengo la kutoa huduma ya muziki wa kiliturujia wakati wa Misa Takatifu na matukio mengine ya Kanisa. Tangu kuanzishwa kwake, kwaya imepitia vizazi kadhaa vya wanakwaya, ikiendelea kukua kiidadi na kiubora wa huduma. Jina la kwaya linaenzi Mt. Stefano, Shahidi wa kwanza wa Kanisa, akiwa mfano wa uaminifu na moyo wa kujitoa. Leo hii, kwaya inaendelea kutumikia kwa kuandaa nyimbo za matukio maalum, kushiriki ziara za kiimbaji ndani na nje ya Jimbo, na kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo ya huduma yake.
Kuhusu Sisi
Historia
